Hamia kwenye habari

Gari la Polisi limeziba njia kwenye daraja katika eneo la Sainte-Marie-de-Beauce, Quebec

MEI 17, 2019
KANADA

Mafuriko Makubwa Yatokea Nchini Kanada

Mafuriko Makubwa Yatokea Nchini Kanada

Maelfu ya watu wanaoishi nchini Kanada katika mikoa ya New Brunswick, Ontario, na Quebec wamepoteza makao kwa sababu ya mafuriko. Katika mkoa wa Quebec pekee, watu 9,000 hivi wamelazimika kuhama nyumba zao.

Ofisi ya tawi ya Kanada imeripoti kwamba katika mkoa wa Quebec, nyumba 44 za ndugu zetu zimeharibiwa. Na katika mikoa ya New Brunswick na Ontario, hakuna ripoti iliyotolewa kuhusu uharibifu lakini mafuriko bado yanaendelea.

Waangalizi wa mzunguko wa maeneo yaliyoathiriwa mkoani Quebec wanashirikiana na wazee wa maeneo hayo kuwatembelea wahubiri katika ziara za uchungaji. Kwa kuongezea, mwakilishi wa ofisi ya tawi alitembelea maeneo yaliyoathiriwa zaidi ili kuwapa utegemezo wa kiroho. Katika eneo la Beauce, ndugu na dada wamemaliza kufanya usafi wa mwanzo na kutoa matope katika nyumba 20 za ndugu zetu. Halmashauri ya Kutoa Msaada ilianzishwa katika eneo la Sainte-Marthe-sur-le-Lac ili kuwasaidia wale ambao nyumba zao ziliharibiwa.

Tunasali kwamba ndugu zetu walioathiriwa na mafuriko hayo wataendelea kumtegemea Yehova, ambaye ndiye ‘nguvu zao na uwezo wao.’—Kutoka 15:2.