NOVEMBA 26, 2021
KANADA
Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko Magharibi mwa Kanada
Novemba 13 hadi 15, 2021, maeneo fulani ya British Columbia, magharibi mwa Kanada yalikumbwa na mvua kubwa. Katika maeneo ishirini, mvua iliyonyesha ndani ya siku mmoja, ilikuwa haijawahi kunyesha kamwe, baadhi ya maeneo hayo yalipata milimita 250 au (inchi 10) za mvua katika siku tatu za dhoruba hiyo. Mvua hizo zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoharibu barabara, pia watu walilazimika kuacha makazi yao na wasafiri walikwama.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Wamepata
Hakuna ndugu aliyejeruhiwa
Wahubiri 144 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 35 hivi ziliharibiwa
Jitihada za Kutoa Msaada
Ofisi ya tawi ya Kanada iliweka rasmi Halmashauri ya Kutoa Msaada (DRC)
Ndugu na dada waliolazimika kuhama walipewa makao na watu wao wa ukoo, na Mashahidi wenzao katika miji ya karibu iliyokuwa salama.
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanafariji familia zilizoathiriwa
Katika maeneo ambayo wenye mamlaka wamesema ni salama, DRC inashirikiana pamoja na vikundi vya Usanifu-Majengo na Ujenzi ili kutathmini kiwango cha uharibifu wa nyumba na kinachohitajika ili kuzirekebisha.
Misaada yote inatolewa kulingana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19
Familia nyingi za Mashahidi zilizoathiriwa na msiba huu, zilikuwa zimelazimika kuhama nyumbani kwa sababu ya moto mkubwa wa msituni uliotokea miezi mitatu tu iliyopita, katika Agosti 2021. Kadiri majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa, na misiba ya asili inavyozidi kuongezeka, watu wa Yehova wamenufaika kwa kutii mwongozo wa kuwa na begi la dharura na chakula cha ziada.
Huenda matatizo yanayosababishwa na misiba yakaongezeka na kuwa mabaya zaidi, tutaendelea kutegemea nguvu za Yehova za kuokoa.—Habakuki 3:17, 18.