Kazakhstan
Mashahidi wa Yehova nchini Kazakhstan
-
Mashahidi wa Yehova—17,287
-
Makutaniko—229
-
Hudhurio kwenye Ukumbusho wa kifo cha Kristo unaofanywa kila mwaka—31,006
-
Uwiano wa Mashahidi wa Yehova kwa kulinganisha na idadi ya watu nchini—1 kwa 1,164
-
Idadi ya watu—19,899,000
Siku 441 za Kifungo—Mahojiano na Teymur na Mafiza Akhmedov
Teymur Akhmedov anaeleza kuhusu kifungo chake Kazakhstan. Alikataa kutenda kinyume na dhamiri yake na alibaki mshikamanifu kwa Yehova.
Teymur Akhmedov Ameachiliwa kwa Msamaha wa Rais
Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev amempa msamaha Teymur Akhmedov, ambaye alikuwa amefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kuwaeleza wengine kuhusu imani yake ya dini. Msamaha huo umefuta rekodi yake ya uhalifu.
Kazakhstan Imepatikana na Hatia ya Kumfunga Isivyo Haki Teymur Akhmedov
Kikundi cha Umoja wa Mataifa Kinachoshughulikia Vifungo Vilivyo Kinyume cha Sheria kimeeleza kwamba Kazakhstan ina hatia ya kumkamata na kumfungulia mashtaka isivyo haki Bw. Akhmedov kwa sababu ya kuwaeleza kwa amani watu wengine mambo anayoamini.
Kazakhstan Imesitisha Utendaji wa Makao Makuu ya Mashahidi Nchini Humo
Mahakama jijini Almaty, Kazakhstan, imesitisha utendaji wa Kituo cha Kikristo cha Mashahidi wa Yehova nchini Kazakhstan kwa miezi mitatu.
Kazakhstan Yamfunga Shahidi wa Yehova Ambaye Ni Mgonjwa na Kupiga Marufuku Ibada Yake
Teymur Akhmedov, mume na baba ya watoto watatu, alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani kwa sababu ya kazi yake ya kufundisha watu Biblia kwa amani.
Kazakhstan Inakandamiza Uhuru wa Ibada na Kumhukumu Teymur Akhmedov
Licha ya hali mbaya ya afya ya Bw Akhmedov, mahakama ya Astana ilimhukumu kifungo cha miaka mitano gerezani kwa sababu ya kuwahubiria wengine kuhusu imani yake.