JULAI 4, 2017
KAZAKHSTAN
Serikali Yasimamisha Utendaji wa Ofisi ya Tawi ya Mashahidi wa Yehova Nchini Kazakhstan
Juni 29, 2017, mahakama ya Kazakhstan iliagiza ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova huko Almaty, Kazakhstan, kukomesha utendaji wake kwa miezi mitatu na kuwapiga faini ya dola 2,107 hivi (680,000 KZT).
Kabla ya uamuzi wa mahakama, wenye mamlaka walivamia ofisi hiyo Mei 17, 2017, jambo lililovutia umati wa watu na kuhusisha kikosi cha askari 40 wenye silaha, baadhi yao wakiwa wamejifunika uso. Mashahidi wanataka kuwasilisha malalamiko kuhusu uvamizi huo.
Juni 5, 2017, polisi walikagua ofisi hiyo na wenye mamlaka wanadai kwamba ukaguzi huo ulionyesha kuwa wamevunja sheria fulani. Mashahidi walikataa matokeo ya ukaguzi huo, ambao uliendeshwa kwa njia iliyo kinyume cha sheria.
Mambo yanayoendelea nchini Kazakhstan yanafanana na vitisho vya polisi na ubaguzi wa kidini dhidi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi, ambako serikali imepiga marufuku utendaji wa Mashahidi wa Yehova. Mashahidi watakata rufaa uamuzi huo wa Juni 29, lazima wafanye hivyo kufikia Julai 14, 2017.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000
Kazakhstan: Bekzat Smagulov, +7-747-671-45-01