Hamia kwenye habari

Jengo la hoteli ya Dusit jijini Nairobi, Kenya, ambako shambulizi lilitokea.

JANUARI 25, 2019
KENYA

Shambulizi Katika Eneo la Hoteli Nchini Kenya

Shambulizi Katika Eneo la Hoteli Nchini Kenya

Januari 15, 2019, watu 21 hivi waliuawa katika shambulizi lililofanywa katika eneo la hoteli na ofisi jijini Nairobi, Kenya.

Ofisi ya tawi ya Kenya inaripoti kwamba hakuna wahubiri waliokufa au kujeruhiwa wakati wa shambulizi hilo lililotokea kilomita saba kutoka kwenye ofisi ya tawi. Zaidi ya ndugu na dada kumi wanafanya kazi katika jengo la Dusit, ambapo shambulizi hilo lilitukia. Wakati wa shambulizi hilo, saba kati yao hawakuwa kazini; wale wengine waliokolewa. Kati ya wale waliookolewa kulikuwa na ndugu mmoja na dada mmoja ambao walijificha kwa saa 12 shambulizi lilipokuwa likiendelea.

Wazee wa eneo hilo pamoja na waangalizi wa mzunguko wanaandaa msaada wa kiroho kwa wahubiri walioathiriwa na msiba huu. Tunasali Yehova aendelee kuwafariji ndugu zetu wakati huu mgumu.—2 Wakorintho 1:3, 4.