APRILI 24, 2017
KOLOMBIA
Maporomoko ya Ardhi Yatokea Kusini mwa Kolombia
Asubuhi ya Jumamosi Aprili 1, 2017, mito mitatu ilivunja kingo zake karibu na jiji la Mocoa, mji mkuu wa mkoa wa Putumayo, Kolombia na kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyowaua mamia ya watu. Kwa kusikitisha, ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Kolombia inaripoti kwamba Mashahidi wawili wa Yehova walikufa katika msiba huyo na mwingine mmoja hajapatikana. Isitoshe, familia tano ziliachwa bila makao. Mashahidi wa Yehova wameanza kazi ya kutoa msaada kwa kuandaa chakula, maji, mafuta, na mahali pa kulala kwa ajili ya walioathiriwa, na wazee wanaandaa msaada wa kiroho. Ofisi ya tawi inaendelea kuangalia hali ile na kuunga mkono kazi ya kutoa msaada inayoendelea.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000
Kolombia: Wilson Torres, +57-1-8911530