Hamia kwenye habari

Ndugu Hye-min Kim akiwa na mke wake, Ha-bin, nje ya Mahakama ya Wilaya ya Gwangju

DESEMBA 7, 2022
KOREA KUSINI

Kesi Yafunguliwa Dhidi ya Utumishi wa Badala wa Kiraia Korea Kusini

Kesi Yafunguliwa Dhidi ya Utumishi wa Badala wa Kiraia Korea Kusini

Mahakam ya Wilaya ya Gwangju iliyo Korea Kusini imepanga kusikiliza kesi ya Ndugu Hye-min Kim Desemba 8, 2022. Hye-min ndiye mtu wa kwanza aliyekataa utumishi wa kijeshi kukataa utumishi wa badala wa kiraia (ACS) kwa sababu ni kama adhabu kali. Kupatana na utumishi huo wa badala alipaswa kufungwa gerezani kwa miezi 36 na pia angekuwa na rekodi ya uhalifu.

Korea Kusini ni moja kati ya nchi zinazotoa utumishi wa badala wa muda mrefu zaidi duniani—yaani, miezi 36, muda ambao ni mara dufu ya muda ambao mtu anatumikia utumishi wa kijeshi. Katika kipindi hicho cha miaka mitatu, watu waliokataa utumishi wa kijeshi wanakuwa katika kifungo kinacholingana na kifungo cha nje lakini kwenye vyumba vilivyo katika eneo la gereza. Wakiwa huko, wanawekewa vizuizi vikali. Hivyo, utumishi huo wa badala unaacha kuwa utumishi wa badala, badala yake wataalamu wa kimataifa wameuita “adhabu ya badala.” a

Katika uamuzi uliofanywa Juni 28, 2018, Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini iligundua kwamba Katiba ya Korea inalinda haki za watu wanaokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri na hivyo iliwatahadharisha wale wanaotunga sheria ili kuwakumbusha hii maana ya utumishi wa badala wa kiraia: “Ikiwa utumish wa badala wa kiraia unakuwa wa muda mrefu sana na mkali sana hivi kwamba watu wanaokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri wanashindwa kuuchagua, basi hilo litakuwa ni kinyume na kusudi ya kuwa na utumishi wa badala, utumishi huo utakuwa sawa na kifungo cha gerezani, kufanya hivyo ni kukiuka haki nyingine za msingi.”

Viwango vya kimataifa vya utumishi wa badala wa kiraia vilianzishwa na Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa katika azimio la mwaka 1998. Nchi ambazo zilikuwa na utumishi wa kijeshi wa lazima zilikumbushwa kwamba zinapaswa kuwapa watu wanaokataa utumishi wa kijeshi wa badala nafasi kwa kufanya utumishi wa aina nyingine ambazo “zitaisaidia jamii na ambazo si kama adhabu.”

Hii sio mara ya kwanza kwa Hye-min kukabiliana na mashtaka ya uhalifu. Septemba 2020, Mahakama Kuu ya Korea Kusini ilimtambua kuwa mtu aliyekataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Majuma kadhaa baadaye, alijaza ombi la kufanya utumishi wa badala. Amesubiri majibu ya ombi hilo hadi Februari 7, 2022. Hata hivyo, baada ya kutambua kwamba mpango huo wa utumishi wa badala wa kiraia ni sawasawa na adhabu kali, aliamua kukataa kufanya utumishi huo kwa heshima.

Ikiwa mahakama itamuunga mkono Hye-min, huenda serikali ya nchi hiyo inaweza kuamua kurekebisha mpango huo wa utumishi wa badala ili ipatane na viwango vya kimataifa. Ikiwa badiliko hilo litafanywa, jamii yao nzima itanufaika na mpango huo na pia ndugu zetu wanaoishi Korea Kusini pamoja na familia zao. Kwa sasa, tunasali kwamba wote wanaoathiriwa na suala hilo waendelee kumtegemea Yehova ili awasaidia “[kuvumilia] kikamili kwa subira na shangwe.”​—Wakolosai 1:11.

a Ili kupata habari zaidi, tafadhali ona ripoti ya pekee yenye kichwa “Utumishi wa Badala wa Kiraia Nchini Korea Kusini” ya Kiingereza, iliyotayarishwa na shirika la Asia-Pacific Association of Jehovah’s Witnesses.