Hamia kwenye habari

Nyumba ya familia fulani ya Mashahidi ambayo iliharibiwa kabisa na moto huo

APRILI 25, 2019
KOREA KUSINI

Moto wa Msituni Wateketeza Eneo la Pwani ya Mashariki ya Korea Kusini

Moto wa Msituni Wateketeza Eneo la Pwani ya Mashariki ya Korea Kusini

Aprili 4, 2019, moto mkubwa wa msituni ulianza kandokando ya pwani ya mashariki ya Korea Kusini katika Mkoa wa Gangwon. Moto huo ulisambaa upesi na kufanya serikali itangaze msiba wa kitaifa. Kabla ya moto huo kudhibitiwa, tayari ulikuwa umeteketeza ekari 4,000 na kuua watu wawili.

Ripoti ya ofisi ya tawi inaonyesha kwamba hakukuwa na ndugu yeyote aliyejeruhiwa au kufa. Hata hivyo, nyumba nane ziliharibiwa, jambo ambalo liliathiri ndugu na dada 27. Halmashauri ya Kutoa Misaada na mwangalizi wa mzunguko wa eneo hilo wakifanya kazi chini ya mwongozo wa ofisi ya tawi wanashirikiana na wazee wa kutaniko kuandaa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa wale walioathiriwa na msiba huo.

Tuna uhakika kwamba Yehova atathibitika kuwa ‘kimbilio na nguvu, msaada unaopatikana kwa urahisi nyakati za taabu’ kwa ajili ya ndugu zetu.—Zaburi 46:1.