Hamia kwenye habari

AGOSTI 30, 2018
KOREA KUSINI

Mahakama Kuu ya Korea Kusini Yasikiliza Hoja Kuhusu Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri

Mahakama Kuu ya Korea Kusini Yasikiliza Hoja Kuhusu Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri

Alhamisi, Agosti 30, 2018, Mahakama Kuu ya Korea Kusini ilisikiliza kesi ya umma iliyohusu Mashahidi wa Yehova watatu ambao walikataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Mambo mengi yamejadiliwa kwa miaka mingi kuhusu kuwafunga gerezani wanaokataa kujiunga na jeshi nchini Korea, kwa hiyo, mahakimu wote 13 waliwauliza mawakili wa Mashahidi na watu wengine maswali kuhusu suala hilo kwa muda wa saa nne. Mahakimu pia walizungumzia kwa kina uamuzi wa kihistoria uliotolewa na Mahakama ya Kikatiba Juni 28, 2018, ambao uliagiza serikali ya Korea iandae utumishi wa badala kwa ajili ya wale ambao kikweli wanakataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri badala ya kuwafunga kama wahalifu. Mawakili waliiomba Mahakama itoe uamuzi wa kutokuwa na hatia katika kisa cha ndugu hao watatu, ili uwe kielelezo cha kuigwa na mahakama za chini zilizo na kesi zaidi ya 900 kama hizo zinazosubiri kutolewa uamuzi. Sasa ni uamuzi wa Mahakama Kuu kujua ni lini na jinsi gani itakavyotoa hukumu katika kesi hizo tatu walizosikiliza.

Tukiwa na uhakika kamili, sisi pamoja na ndugu waaminifu zaidi ya 100 walio gerezani tunaendelea kumngoja kwa subira Mungu wa wokovu wetu.—Mika 7:7.