Hamia kwenye habari

NOVEMBA 30, 2018
KOREA KUSINI

Ndugu Nchini Korea Waachiliwa Kutoka Gerezani

Ndugu Nchini Korea Waachiliwa Kutoka Gerezani

Ofisi ya tawi ya Korea inaripoti kwamba Novemba 30, 2018, ndugu 57 waliachiliwa kutoka gerezani na kuungana tena na familia zao. Ndugu ulimwenguni pote wanafurahia sana tukio hilo walilosubiri kwa hamu na wanamsifu Yehova kwa kuwapa kibali na baraka zake.—Hesabu 6:24-26.

Tunasali kwa ajili ya ndugu nane waliosalia gerezani ambao wanatarajia kuachiliwa baada ya kutumikia miezi 6 ya kifungo chao cha miezi 18.

Ndugu walioachiliwa hivi karibuni wakiungana na wazazi wao(kushoto, kulia). Ndugu akihojiwa na wanahabari nje ya gereza (katikati).