Hamia kwenye habari

JUNI 28, 2018
KOREA KUSINI

Uamuzi wa Kihistoria wa Mahakama ya Katiba Nchini Korea: Ni Kinyume cha Sheria Kutokuwa na Utumishi wa Badala wa Kiraia

Uamuzi wa Kihistoria wa Mahakama ya Katiba Nchini Korea: Ni Kinyume cha Sheria Kutokuwa na Utumishi wa Badala wa Kiraia

Juni 28, 2018, kwa mara ya kwanza katika historia ya Korea Kusini, Mahakama ya Katiba ilisema kwamba sehemu fulani ya Sheria ya Utumishi wa Kijeshi Nchini Korea (MSA) ni kinyume cha sheria, kwa kuwa haihusishi utumishi badala kwa wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Uamuzi huo ni muhimu sana katika kubadili sera ya miaka 65 ya kuwafunga wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

Tangu mwaka wa 1953, ndugu zetu zaidi ya 19,300 wamehukumiwa jumla ya miaka zaidi ya 36,700 gerezani. Uamuzi huo unaandaa njia kwa Mahakama Kuu ya Korea kuutumia katika visa vinavyohusisha wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Isitoshe, watunga sheria nchini Korea sasa wanalazimika kuanzisha utumishi wa badala wa kiraia kwa ajili ya wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri kufikia Desemba 31, 2019.

Sote tunashangilia pamoja na ndugu zetu nchini Korea kwamba kuna msingi wa kukomesha ukosefu wa haki ulioendelea kwa miaka mingi sana.—Methali 15:30.