Hamia kwenye habari

Majengo yaliyoharibiwa sana katika mtaa wa Petrinja, Kroatia

JANUARI 8, 2021
KROATIA

Tetemeko Kubwa la Ardhi Lapiga Kroatia

Tetemeko Kubwa la Ardhi Lapiga Kroatia

Mahali

Karibu na mji wa Petrinja, uliopo kilomita 50 kusini mwa Zagreb, Kroatia

Janga

  • Desemba 29, 2020, Kroatia ilipigwa na tetemeko kubwa la ardhi. Tetemeko hilo linatajwa kuwa kubwa zaidi lililowahi kutokea Kroatia

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri wote 91 katika eneo hilo hawakujeruhiwa

  • Wahubiri 29 walilazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa mali

  • Nyumba 9 zimepata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 16 ziliharibiwa kidogo

  • Jumba la Ufalme katika eneo la Sisak lilipata uharibifu kidogo

Jitihada za kutoa msaada

  • Ofisi ya tawi ya Kroatia imeweka rasmi Halmashauri ya Kutoa Msaada. Huku wakifuata miongozo yote ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, halmashauri hiyo inashirikiana na waangalizi wawili wa mzunguko na wazee wa kutaniko katika eneo hilo ili kutoa msaada wa kiroho na wa kimwili unaotia ndani kutafuta makazi ya muda kwa ajili ya waliolazimika kuhama makazi yao

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwapa ndugu zetu nguvu wanazohitaji katika kipindi hiki kigumu.—1 Petro 5:10.