Hamia kwenye habari

FEBRUARI 2, 2022
MADAGASKA

Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko Nchini Madagaska

Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko Nchini Madagaska

Januari 2022, mvua kubwa zilisababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi, na kuangusha majengo jijini Antananarivo, mji mkuu wa Madagaska. Inatarajiwa kwamba mvua hizo zitaendelea.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada yetu aliyejeruhiwa au kufa

  • Wahubiri 693 hivi wamelazimika kuhama makao yao

  • Hakuna Majumba ya Ufalme yaliyoharibiwa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri ya Tawi imeanzisha Halmashauri ya Kutoa Msaada (DRC) itakayosimamia kazi ya kutoa msaada kupatana na miongozo ya kujilinda na COVID-19.

  • DRC, waangalizi wa mzunguko, na wazee wa eneo hilo wanawasaidia ndugu zetu kiroho na kimwili kwa kupanga mahali pa kulala pa muda, chakula, na mahitaji mengine

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea “ngome” kwa ajili ya ndugu zetu wakati huu mgumu.​—Zaburi 31:2.