Hamia kwenye habari

JANUARI 25, 2018
MADAGASKA

Tufani Ava Yaipiga Madagaska

Tufani Ava Yaipiga Madagaska

Hali nchini Madagaska inaanza kutulia baada ya Tufani Ava kuipiga nchi hiyo Januari 5, 2018. Maofisa wameripoti kwamba watu 51 hivi wamekufa na maelfu wameachwa bila makao.

Ripoti za sasa kutoka kwenye ofisi ya tawi ya Madagaska zinaonyesha kwamba hakuna ndugu waliokufa kutokana na tufani hiyo. Hata hivyo, nyumba 45 na Majumba 6 ya Ufalme yaliharibiwa. Pia, tufani hiyo iliharibu mazao yote ambayo ndiyo riziki ya wahubiri wengi nchini humo. Halmashauri ya Kutoa Msaada Wakati wa Misiba ilifanyizwa ili kushughulikia mahitaji ya sasa ya wahubiri walioathiriwa, yanayotia ndani chakula, mavazi, na makao ya muda. Ndugu wawili kutoka kwenye ofisi ya tawi walisafiri kwenda kwenye eneo la msiba na wakawa na mkutano wa pekee pamoja na familia za walioathiriwa ili kuwatia moyo kupitia maandiko.

Baraza Linaloongoza husimamia kazi ya kutoa msaada wakati wa misiba, kutia ndani kazi inayoendelea sasa baada ya tufani hiyo. Linafanya hivyo kupitia michango inayotolewa kwa ajili ya kazi ya Mashahidi ya kuhubiri ulimwenguni pote. Tunasali kwamba Yehova ataendelea kuwa kimbilio salama kwa ajili ya ndugu na dada zetu nchini Madagaska katika kipindi hiki.—Zaburi 9:9, 10

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Madagaska: Rinera Rakotomalala, +261-33-37-012-91