Matukio Muhimu Kihistoria Katika Maeneo ya Palestina
JANUARI 2014—Wenye mamlaka nchini Palestina walikubali kuwapatia watoto wa Mashahidi vyeti vya kuzaliwa baada ya kukataa kufanya hivyo mara kadhaa
OKTOBA 2, 2013—Mahakama Kuu ya Ramallah yakataa ombi la kusajiliwa kisheria la Mashahidi
SEPTEMBA 20, 2010—Ombi la kusajiliwa kisheria latumwa tena; majibu hayakurudishwa
AGOSTI 4, 1999—Maombi ya kutambuliwa kisheria yatumwa kwa rais wa Mamlaka ya Palestina lakini hayakushughulikiwa
1967—Makutaniko mawili yaliyokuwa katika eneo la Jordan yawa sehemu ya eneo la West Bank nchini Israel
1948—Baada ya vita vya Palestina na Israel, makutaniko mawili ya kwanza yaliyokuwa Palestina yakawa sehemu ya Jordan
1920—Kutaniko la kwanza la Mashahidi wa Yehova laanzishwa Ramallah
1891—Msimamizi wa kwanza wa Watch Tower Society, Charles T. Russell, atembelea Palestina