Hamia kwenye habari

Dhoruba zaikumba California, Marekani na kuacha uharibifu mkubwa

JANUARI 19, 2023
MAREKANI

Dhoruba Hatari Zatokea Magharibi ya Marekani

Dhoruba Hatari Zatokea Magharibi ya Marekani

Kuanzia Januari 4, 2023, theluji nyingi, mvua kubwa, na upepo mkali ulisababisha madhara kule California, Marekani. Dhoruba hizo zilizoendelea bila kuacha zimesababisha mafuriko, maporomoko ya matope, na kukatiza umeme. Maelfu ya watu wamelazimika kuhama nyumba zao na watu 19 hivi wamekufa. Dhoruba hizo zilikumba maeneo fulani sana hivi kwamba ndani ya siku chache maeneo hayo yalipata kiasi cha mvua ambacho kawaida kinanyesha kwa nusu mwaka.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada yetu ambaye alikufa

  • Wahubiri 199 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 4 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 141 zilipata uharibifu mdogo

  • Majumba 23 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

  • Ofisi 1 ya utafsiri ilipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo wanafanya ziara za uchungaji kwa familia zilizoathiriwa na kutoa msaada mwingine unaohitajika

  • Nyumba 44 zimefanyiwa ukarabati wa kuziimarisha

  • Nyumba 15 zimefanyiwa marekebisho

Tuna uhakika kwamba Yehova anawafariji ndugu zetu wakati huu wa taabu.​—Zaburi 50:15.