Hamia kwenye habari

MEI 13, 2014
MAREKANI

Dhoruba Kali Zapiga Kusini na Katikati mwa Marekani

Dhoruba Kali Zapiga Kusini na Katikati mwa Marekani

Kuanzia Aprili 27, 2014, hali mbaya ya hewa ilisababisha dhoruba kali za upepo katikati na kusini mwa Marekani. Dhoruba hizo zilibomoa nyumba, na ripoti mbalimbali zinasema kwamba zaidi ya watu 30 walikufa. Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova imeripoti kwamba hakuna Shahidi hata mmoja aliyekufa au kujeruhiwa kutokana na msiba huo, lakini nyumba saba ziliharibiwa. Pia, majumba matatu ambayo Mashahidi huyatumia kwa ajili ya ibada yaliharibiwa. Mashahidi wa eneo hilo waliojitolea wanafanya kazi katika halmashauri mbalimbali ili kuwasaidia wale walioathiriwa na dhoruba hizo.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000