Hamia kwenye habari

JANUARI 13, 2020
MAREKANI

Habari za Karibuni: Kazi ya Kutoa Msaada Baada ya Kimbunga Dorian

Mashua na Ndege Zaleta Msaada

Habari za Karibuni: Kazi ya Kutoa Msaada Baada ya Kimbunga Dorian

Kimbunga Dorian kilipiga Bahamas kuanzia Septemba 1 hadi Septemba 3, 2019. Hata kabla ya kimbunga hicho kupiga, ofisi ya tawi ya Marekani mipango ya kutoa msaada huko Florida, Marekani. Hali ya hewa ilipokuwa shwari kwa ajili ya kusafiri, ndugu dada waliomiliki ndege na mashua, waliombwa kupeleka misaada na kuwa kati ya wajitoleaji wa kwanza kutoa msaada

Ndugu na dada kumi na watatu walisafirisha tani 15 za mahitaji ya msingi na wajitoleaji zaidi ya 700 kwa ndege, na kuzifikisha kwenye vituo 300 katika sehemu zilizoathiriwa na kimbunga hicho. Kwa kuongezea, mashua 13 za ndugu zetu zilitumika kusafirisha karibu tani 90 za mahitaji ya msingi. Kwa wastani, safari moja ya kwenda na kurudi tokea Florida ilichukua masaa 12.

Jose Cabrera, msimamizi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Palm Beach iliyopo Florida alisema hivi: “Pindi Kimbunga kilipopita tu, ndege [za Mashahidi] zilikuwa zikipaa angani, zikibeba mahitaji, na zikiwa tayari kutoa msaada. Wamefanya yote wawezayo.”

Ndugu Glenn Sanders, aliye mmoja kati ya marubani waliojitolea kusaidia alisema hivi: “Kwa wengi wetu, hii ilikuwa mara yetu ya kwanza kutumia ujuzi tulionao ili kuwasaidia ndugu na dada zetu. Tulihisi vizuri kujua kwamba tukiwa kiungo kidogo cha mwili, sehemu ndogo ya mwili, tumepeleka msaada kwa kiungo kingine cha mwili kilichoumia.”—1 Wakorintho 12:26.

Ofisi ya tawi ya Marekani inakadiria kwamba, pesa zitakazotumika katika zoezi hilo la kutoa msaada zitafikia takriban dola za Marekani 1,750,000 na zoezi hilo litamalizika ifikapo Mei 1, 2020.

 

Mahitaji mbalimbali ya msingi ikipakizwa kwenye mashua huko Florida, Marekani. Ndugu zetu walienda safari 29 kuelekea Bahamas kwa mashua

Picha ya uwanja wa ndege uliojaa maji katika kisiwa cha Great Abaco, nchini Bahamas

Picha iliyochukuliwa na rubani wakati wa safari