Hamia kwenye habari

Madhara ya dhoruba iliyopiga eneo la El Reno, Oklahoma

JUNI 13, 2019
MAREKANI

Hali Mbaya ya Hewa Imeathiri Sehemu Mbalimbali za Marekani

Hali Mbaya ya Hewa Imeathiri Sehemu Mbalimbali za Marekani

Mei 2019, taarifa za habari zimeripoti kuwa Marekani imekumbwa na mvua kubwa na dhoruba 500 hivi.

Mashahidi wa Yehova wa Arkansas, Indiana, Mississippi, Missouri, Ohio, Oklahoma, Pennsylvania, na Texas waliathiriwa na hali hiyo ya hewa. Hakuna ndugu au dada aliyekufa. Lakini sita kati yao wamejeruhiwa na dhoruba hiyo, na wanne kati ya hao sita wamelazwa hospitalini. Kwa kuongezea, nyumba 6 za ndugu zetu ziliharibiwa kabisa na nyumba nyingine 98 pamoja na Majumba ya Ufalme 12 yameharibiwa kwa kiwango fulani. Kwa kuwa nyumba nyingi zimeharibiwa, waabudu wenzetu 84 hawana makao.

Akina ndugu wanapoendelea kutathmini uharibifu, wanawapatia chakula, maji, na makao wale walioathiriwa na janga hilo. Wazee wa makutaniko ya maeneo hayo na waangalizi wa mzunguko wanaendelea kushughulikia mahitaji ya kiroho na ya kihisia ya ndugu zetu.

Tutaendelea kuwategemeza na kusali kwa ajili ya waabudu wenzetu, wanapoendelea kukabiliana na matokeo ya dhoruba hizo.—2 Wakorintho 1:3, 4.