Hamia kwenye habari

JULAI 22, 2019
MAREKANI

Kimbunga Barry Chapiga Kusini mwa Marekani

Kimbunga Barry Chapiga Kusini mwa Marekani

Siku ya Jumamosi, Julai 13, 2019, upepo mkali ulisababisha mvua katika jimbo la Louisiana, baadaye mvua ilipungua na upepo huo ulisababisha kimbunga kinachojulikana kama Barry. Kimbunga hiki kilisababisha uharibifu kwa sababu ya upepo na mafuriko, pia kilisababisha kukatika kwa umeme katika majimbo ya Alabama, Louisiana, na Mississippi.

Ingawa hakuna mhubiri hata mmoja aliyejeruhiwa au kufa kwa sababu ya kimbunga hiki, wahubiri 123 walihama kutoka katika makazi yao. Isitoshe, kimbunga kiliharibu nyumba 27 za akina ndugu na dada, pamoja na Majumba ya Ufalme matano.

Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanawatembelea na kuwatia moyo wale wote walioathiriwa na kimbunga hicho. Pia, wahubiri katika makutaniko ya jirani wametoa msaada wa maji, chakula, na makazi kwa ndugu na dada wenye uhitaji. Ndugu wanaendelea kujitahidi kufanya ukarabati na marekebisho madogo-madogo.

Tutaendelea kuwakumbuka katika sala na kuwategemeza ndugu na dada wa eneo hilo la kusini mwa Marekani ambao wameathiriwa na kimbunga Barry.—Methali 18:10.