Hamia kwenye habari

AGOSTI 6, 2020
MAREKANI

Kimbunga Hanna Chasababisha Uharibifu Kusini-Mashariki mwa Texas

Kimbunga Hanna Chasababisha Uharibifu Kusini-Mashariki mwa Texas

Mahali

Texas, Marekani

Janga

  • Julai 25, 2020, upepo mkali ulisababisha mvua kubwa na mafuriko, na mawimbi makubwa baharini

  • Hanna ni kimbunga cha kwanza kutokea katika msimu wa vimbunga vinavyosababishwa na bahari ya Atlantiki

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Ndugu zetu wawili wamepata majeraha madogo

  • Wahubiri 193 wamelazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa Mali

  • Nyumba 347 za ndugu zetu zimeharibiwa kidogo

  • Nyumba 31 zimepata uharibifu mkubwa

Jitihada za kutoa msaada

  • Waangalizi wa mzunguko katika maeneo yaliyoathiriwa wanashirikiana na wazee wa makutaniko ili kuandaa msaada wa kiroho na wa kimwili.

Tunamshukuru Yehova, “Mungu wa faraja yote” anayendelea kuwatunza ndugu na dada zetu walio Texas katika kipindi hiki kigumu.—2 Wakorintho 1:3, 4.