SEPTEMBA 8, 2021
MAREKANI
Kimbunga Ida Chaikumba Marekani Kuanzia Kusini Hadi Kaskazini
Agosti 29, 2021, Kimbunga Ida kilipiga nchi kavu karibu na eneo la Port Fourchon, Louisiana. Dhoruba kali, mvua kubwa, na upepo mkali ulisababisha mafuriko, uharibifu wa mali, na ukosefu wa umeme katika eneo lote la Marekani linaloitwa Gulf Coast. Septemba 1 masalio ya Kimbunga Ida yalisababisha marufiko ya ghafla na vimbunga katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Marekani. Katika maeneo fulani, inakadiriwa kwamba umeme utarudishwa baada ya majuma kadhaa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Kufikia sasa hatujapata ripoti kwamba yeyote amekufa
Ndugu 2 walipata majeraha madogo
Dada 1 alilazwa hospitalini kwa sababu ya jeraha ambalo alipata alipokuwa akiondoka nyumbani kwake
Nyumba 1,429 zimeharibiwa kidogo
Nyumba 183 zimepata uharibifu mkubwa
Nyumba 19 zimeharibiwa kabisa
Majumba 43 ya Ufalme yameharibwa kidogo
Majumba 10 ya Ufalme yamepata uharibifu mkubwa
Majumba 4 ya Kusanyiko yamepata uharibifu mkubwa
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa maeneo hayo pamoja Halmashauri za Kutoa Msaada wanafanya ziara za uchungaji kwa ndugu na dada walioathiriwa
Msaada wa kibinadamu unatolewa kwa wale walio na mahitaji ya dharura
Jitihada za kutoa msaada zinatolewa kupatana na miongozo ya usalama ya COVID-19
Kwa kuwa ndugu zetu walikuwa wamejitayarisha kwa ajili ya misiba na pia kushirikiana kwao na miongozo ya serikali ya kuhama maeneo yaliyokuwa hatari kumesaidia kuokoa uhai.—Methali 22:3.