Hamia kwenye habari

AGOSTI 14, 2020
MAREKANI

Kimbunga Isaias Chasababisha Uharibifu Mkubwa Mashariki ya Marekani

Kimbunga Isaias Chasababisha Uharibifu Mkubwa Mashariki ya Marekani

Mahali

Mashariki ya Marekani

Janga

  • Agosti 3, 2020, kimbunga Isaias kilisababisha uharibifu mkubwa katika jimbo la North Carolina

  • Kimbunga kilitokeza vimbunga vingi kadiri kilipokuwa kikielekea Pwani ya Mashariki, na kusababisha upepo mkubwa ulioharibu mali na kukatika kwa umeme

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Dada mmoja amepata majeraha

  • Familia 12 zimelazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa Mali

  • Nyumba 55 za ndugu zetu zimeharibiwa kidogo

  • Nyumba 5 zimepata uharibifu mkubwa

  • Magari kadhaa yameharibiwa

  • Majumba ya Ufalme matano yameharibiwa kidogo

Jitihada za kutoa msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko walio katika maeneo yaliyoathiriwa na janga hilo waliungana mara moja na kuwasaidia ndugu na dada zetu huku wakizingatia miongozo wa jinsi ya kujilinda na ugonjwa wa COVID-19

Tunafurahi kwamba Yehova anaendelea kuwategemeza na kuwalinda ndugu na dada zetu walioathiriwa na dhoruba hiyo kali. Tunatazamia kwa hamu wakati ambapo kila mmoja wetu “hatahangaishwa na woga wa msiba” unaoletwa na majanga ya asili.—Methali 1:33.