Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 7, 2020
MAREKANI

Kimbunga Laura Chaikumba Louisiana

Kimbunga Laura Chaikumba Louisiana

Eneo

Arkansas, Mississippi, Louisiana magharibi, na Texas mashariki

Janga

  • Agosti 27, 2020 Kimbunga Laura kilichokuwa na nguvu nyingi kilipiga eneo la Louisiana magharibi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kukata umeme katika sehemu kubwa.

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Tunasikitika kuripoti kwamba dada mmoja mwenye umri mkubwa alikufa alipokuwa akiokolewa kutoka kwenye kituo cha afya

  • Dada mwingine alipata jereha dogo

  • Wahubiri 3,992 walilazimika kuondoka nyumbani kwao kwa muda fulani

Uharibifu wa mali

  • Nyumba 10 za ndugu zetu ziliharibiwa

  • Nyumba 95 na Majumba 4 ya Ufalme yaliharibiwa kwa kadiri kubwa

  • Nyumba 192 na Majumba 16 ya Ufalme yaliharibika kwa kadiri ndogo

Jitihada za kutoa msaada

  • Ofisi ya tawi ya Marekani imeanzisha Halmashauri ya Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo wanaendelea kuwasaidia wahubiri kupata mahali salama pa kulala katika kipindi hiki ambacho hawawezi kurudi kwao

Mambo yaliyoonwa

  • Ndugu katika maeneo jirani waliwakaribisha wengine nyumbani kwao, huku wakidumisha tahadhari za afya zinazohusiana na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Ndugu mmoja aliyeokolewa anasema hivi: “Mambo yote haya yanatuonyesha baraka za Yehova!”

Kwa kutii mwongozo na kuwasaidia wengine walio na uhitaji, ndugu na dada zetu katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho “[wanajipendekeza] kuwa wahudumu wa Mungu.”—2 Wakorintho 6:4.