Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 24, 2020
MAREKANI

Kimbunga Sally Chasababisha Mafuriko Kusini-Mashariki mwa Marekani

Kimbunga Sally Chasababisha Mafuriko Kusini-Mashariki mwa Marekani

Eneo

 

Alabama, Florida, na Mississippi

Janga

  • Septemba 16, 2020, upepo mkali ulisababisha mvua kubwa katika eneo la Alabama. Mvua hiyo iliendelea kunyesha kwa saa kadhaa, na kusababisha mafuriko makubwa.

  • Upepo mkali uliharibu vibaya sana mali na kusababisha umeme ukatike katika maeneo mengi

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri 240 wamelazimika kuhama makazi yao

  • Mhubiri 1 alijeruhiwa kidogo

Uharibifu wa mali

  • Nyumba 143 na Majumba ya Ufalme 11 yaliharibiwa kidogo

  • Nyumba 12 na Jumba la Ufalme 1 limepata uharibifu mkubwa

Jitihada za kutoa msaada

  • Halmashauri mbili za Kutoa Msaada katika eneo hilo zinashirikiana na waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa ili kuwaandalia ndugu na dada mahitaji yao ya kiroho na kimwili, wakati uleule wakizingatia miongozo ya kujilinda na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19)

Mhubiri mmoja alikiri kwamba aliathiriwa sana kihisia baada ya janga hilo kutokea. Hata hivyo, baada ya kutaniko kumpa msaada bila kuchelewa, anasema hivi akiwa na shukrani moyoni, “Ninaguswa hisia sana ninapoona upendo na utegemezi ninaopata kutoka kwa ndugu na dada zangu.”—1 Yohana 3:18.