NOVEMBA 6, 2020
MAREKANI
Kimbunga Zeta Chasababisha Uharibifu Kusini-Mashariki mwa Marekani
Eneo
Kusini-mashariki mwa Marekani
Janga
Oktoba 28, 2020 upepo mkali ulisababisha mvua kubwa katika eneo la Louisiana. Upepo huo ulipungua na kuwa dhoruba ya kitropiki iliyoathiri maeneo mengi ya kusini-mashariki mwa Marekani
Dhoruba na pepo kali katika maeneo ya pwani ziliharibu mali na kusababisha umeme kukatika
Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata
Wahubiri 324 wamelazimika kuhama makazi yao
Mhubiri 1 amejeruhiwa kidogo
Uharibifu wa mali
Nyumba 291 na Majumba 14 ya Ufalme yaliharibiwa kidogo
Nyumba 8 na Majumba 3 ya Ufalme yaliharibiwa kwa kadiri kubwa
Nyumba 1 iliharibiwa kabisa
Jitihada za kutoa msaada
Wazee na waangalizi wa mzunguko wa eneo hilo wanatoa msaada wa kiroho kupitia uchungaji na msaada wa kimwili kwa ndugu na dada walioathiriwa na janga hilo. Halmashauri za Kutoa Misaada zilizopewa daraka la kutoa msaada wakati wa Kimbunga Laura na kwa ajili ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) katika eneo hilo, zinatoa pia msaada kwa walioathiriwa na Kimbunga Zeta, huku wakizingatia miongozo ya kujilinda na COVID-19.
Tunasikitika kusikia kwamba kimbunga hicho kimeathiri ndugu na dada zetu. Hata hivyo, kwa mara nyingine tena, upendo mshikamanifu wa Yehova kuelekea waabudu wake unaonekana kupitia kazi ya kutoa msaada inayofanywa na ndugu na dada zetu.—Zaburi 89:1.