Hamia kwenye habari

Magari yakiwa yametapakaa kwenye barabara kuu ya Interstate 45, huko Houston, Texas

OKTOBA 2, 2019
MAREKANI

Kimbunga cha Kitropiki Chasababisha Mafuriko Makubwa Kusini Mashariki mwa Texas

Kimbunga cha Kitropiki Chasababisha Mafuriko Makubwa Kusini Mashariki mwa Texas

Katika juma la Septemba 16, 2019, Kimbunga cha Kitropiki kiitwacho Imelda kilileta mafuriko katika sehemu fulani za kusini mashariki mwa Texas kutokana na mvua nyingi iliyonyesha kwa muda wa siku chache tu. Inasemekana kwamba ndicho kimbunga chenye mvua nyingi zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani. Baada ya kimbunga hicho, mamia ya magari yalitapakaa kwenye barabara kuu na barabara nyinginezo. Wakaaji wengi walilazimika kuhamishwa.

Ripoti za mwanzoni kutoka kwa ofisi ya tawi ya Marekani zinaonyesha kwamba hakuna yeyote kati ya akina ndugu 29,649 katika maeneo yaliyoathiriwa ambaye alijeruhiwa au kufa. Hata hivyo, wahubiri 114 walilazimika kuhama. Isitoshe, nyumba 145 za akina ndugu zetu ziliharibiwa. Majumba ya Ufalme kumi yaliharibiwa pia.

Ofisi ya tawi imeunda Halmashauri ya Kutoa Msaada ambayo inashirikiana kwa ukaribu na waangalizi wa mzunguko na wazee katika eneo hilo ili kutambua kiwango cha uharibifu uliotokea na kusimamia mipango ya kutoa msaada. Tunajua kwamba Yehova atawasaidia ndugu zetu, kwa kuwa “upendo [wake] mshikamanifu unafika mpaka mbinguni.”—Zaburi 36:5.