Hamia kwenye habari

AGOSTI 27, 2021
MAREKANI

Mafuriko ya Ghafla Yakumba Eneo la Gila Bend, Arizona

Mafuriko ya Ghafla Yakumba Eneo la Gila Bend, Arizona

Usiku wa Agosti 13, 2021, dhoruba kubwa ilitokeza mvua kubwa na mafuriko makubwa katika maeneo fulani ya Arizona na magharibi mwa Texas. Mafuriko hayo makubwa yaliathiri sana mji wa Gila Bend, Arizona.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Kwa kusikitisha, dada 1 alikufa kutokana na msiba huo

  • Nyumba 5 za ndugu zetu zimepata uharibifu mkubwa

  • Familia 3 zimelazimika kuhama makazi yao

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Mwangalizi wa mzunguko na wazee wa maeneo hayo wanafanya ziara za uchungaji na kusaidia kupanga makao ya muda kwa ajili ya waliolazimika kuhama makazi yao

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya usalama ya COVID-19

Tunasali kwa ajili ya wale ambao wameathiriwa na msiba huo. Yehova na aendelee kuifariji familia ya dada yetu mpendwa aliyekufa.—2 Wakorintho 1:3, 4.