Hamia kwenye habari

Eneo la shambulizi, jengo la manispaa jijini Virginia Beach

JUNI 4, 2019
MAREKANI

Mauaji Jijini Virginia Beach, Marekani

Mauaji Jijini Virginia Beach, Marekani

Mei 31, 2019, mtu mwenye bunduki aliwapiga risasi wafanyakazi wa jengo la ofisi ya manispaa katika eneo la Virginia Beach, Virginia, Marekani. Watu kumi na wawili waliuawa na wanne walijeruhiwa.

Ofisi ya tawi ya Marekani inaripoti kwamba inasikitisha kwamba dada anayeitwa, LaQuita Brown, aliuawa katika shambulizi hilo. Dada Brown alikuwa na umri wa miaka 39 na alikuwa painia wa kawaida katika Kutaniko la Seaview French huko Norfolk, Virginia. Pia alikuwa mjitoleaji katika Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi. Wazee wa eneo hilo na mwangalizi wa mzunguko wanawategemeza kihisia washiriki wa familia ya Dada Brown na rafiki zake na kuwatia moyo kupitia Maandiko.

Tunasikitika sana kumpoteza dada yetu. Tunatazamia kwa hamu wakati ambapo misiba kama hii haitakuwepo na kutakuwa na “wingi wa amani.”—Zaburi 37:10, 11.