JULAI 12, 2019
MAREKANI
Miami, Marekani (Kiingereza)—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe!”
Tarehe: Julai 5-7, 2019
Mahali: Marlins Park Miami, Florida, Marekani
Lugha za Programu: Kiingereza, Kichina cha Mandarini
Idadi ya Wahudhuriaji: 28,000
Idadi ya Waliobatizwa: 181
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Brazili, Uingereza, Kanada, Kolombia, Jamhuri ya Dominika, Fiji, Ghana, Ugiriki, Hong Kong, Israel, Japani, Uholanzi, Skandinavia, Afrika Kusini, Hispania, Taiwan, Trinidad na Tobago, Ukrainia
Mambo Yaliyoonwa: Francis X. Suarez, meya wa jiji la Miami, alitembelea eneo la kusanyiko Jumapili na kusema: “Nimependa ujumbe unaowasilishwa, ‘Upendo Haushindwi Kamwe’!” Kisha aliongezea kwa kusema: “Ni ujumbe mzuri sana, nafikiri kusanyiko kama hili ni zuri sana kwa mji wowote mkubwa uliopo Marekani au popote duniani.”
Watoto wakisaidia kuwakaribisha wajumbe kwenye uwanja wa ndege wa Miami
Wajumbe wakishirikiana na wenyeji kukaribisha majirani kusanyikoni
Wajumbe wakipokea nakala za Tafsiri ya Ulimwengu Mpya iliyorekebishwa katika Kichina, ambayo ilitolewa siku ya Ijumaa
Wajumbe wakiandika mambo makuu kusanyikoni
Dada watatu kati ya ndugu na dada 181 wakibatizwa
Ndugu na dada wenyeji wakiwasalimia wajumbe na kupeana zawadi
Wamishionari na wanabetheli wanaotumikia katika nchi za kigeni wakiwapungia mkono wahudhuriaji siku ya Jumapili alasiri
Ndugu Lösch akisalimia watumishi wa wakati wote siku ya Jumapili
Watoto wakiwaburudisha wajumbe kwa wimbo wakati wa tafrija ya jioni