APRILI 28, 2021
MAREKANI
Mlima wa Volkano Wawafanya Watu Wahame Katika Eneo la Karibea
Mahali
Maeneo ya St. Vincent na Barbados
Janga
Aprili 9, 2021, Mlima La Soufrière wa volkano ulianza kutokeza majivu na moshi
Majivu mazito yaliangusha majengo na kukatiza huduma za umeme na maji na kuwaacha watu wakiwa na kiasi kidogo sana cha maji
Mlipuko huo wa volkano unatarajiwa kuendelea, huenda kwa majuma kadhaa
Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata
Wahubiri 185 walio St. Vincent na Barbados walihamishwa
Uharibifu wa mali
Eneo lililoathiriwa zaidi katika eneo la kaskazini la St. Vincent bado haliwezi kufikika; uharibifu bado haujakadiriwa
Jitihada za kutoa msaada
Ndugu na dada waliohamishwa wanakaribishwa katika nyumba za Mashahidi wenzao wanaoishi katika maeneo salama zaidi kwenye kisiwa cha St. Vincent na visiwa vingine vya karibu, huku wote wakifuata tahadhari za ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19)
Halmashauri ya Kutoa Msaada ya COVID-19 katika eneo hilo ilipewa mgawo wa kusaidia katika jitihada za kutoa msaada wa janga hili pia. Halmashauri hiyo inafanya kazi pamoja na mwangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo kuandaa maji ya kunywa na kuwasaidia wanaohitaji kuhamishwa
Maofisa wa St. Vincent na St. Lucia wamesaidia pia katika kazi ya kutoa msaada
Ndugu mmoja mwenye umri mkubwa ambaye pia ni kipofu na anayeishi peke yake katika eneo lililoathiriwa aliokolewa na kikundi cha akina ndugu kabla tu ya mlipuko huo kuanza. Walipokuwa wakisafiri kwenda eneo salama zaidi, akina ndugu hao walijionea watu walipokuwa wakikimbia. Inapendeza kwamba wahubiri wote walihamishwa wakiwa salama.
Tunafurahi kwamba jitihada za kutoa msaada zimewasaidia ndugu na dada zetu kupata mahali pa kukimbilia na kupata faraja kwa kumwiga Mungu wetu ambaye ni “msaada unaopatikana kwa urahisi nyakati za taabu.”—Zaburi 46:1-3.