AGOSTI 15, 2019
MAREKANI
Phoenix, Marekani—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe: Agosti 9-11, 2019
Mahali: Chase Field, Phoenix, Arizona, Marekani
Lugha ya Programu: Kiingereza
Idadi ya Wahudhuriaji: 40,237
Idadi ya Waliobatizwa: 352
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Uingereza, Kanada, Ulaya ya Kati, Chile, Ufaransa, Ugiriki, India, Italia, Korea, Micronesia, Skandinavia, Sri Lanka, Tahiti, Thailand, Trinidad na Tobago, Uturuki
Mambo Yaliyoonwa: Steve Moore, rais na mkurugenzi wa kampuni ya Visit Phoenix, ambayo ilisaidia kupanga makusanyiko na hoteli katika eneo la Phoenix alisema hivi: “Kwa muda mrefu ambao nimefanya kazi hii, [kusanyiko hili] ndilo kusanyiko pekee ambalo mambo yalifanywa kwa utaratibu mzuri sana. Nimefurahia sana kufanya kazi nanyi. Na pamoja na mambo hayo yote, mliahidi kwamba mngesafisha uwanja kabla ya kuondoka—hakuna mtu yeyote anayefanya hivyo.”
Wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakikaribishwa kwa uchangamfu walipofika kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sky Harbor jijini Phoenix
Ndugu na dada kutoka Phoenix wakiwa tayari kuwapokea wajumbe kwenye mojawapo ya hoteli
Mamia ya ndugu na dada wakiwasalimu wajumbe kwa shauku walipowasili kwenye uwanja wa kusanyiko wa Chase Field siku ya Ijumaa asubuhi
Wajumbe, baadhi yao wakiwa wamevaa mavazi ya asili wakisikiliza programu
Wahubiri wawili wapya kati ya 352 waliobatizwa
Ndugu Samuel Herd, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho katika siku ya pili ya kusanyiko
Wajumbe wakipiga picha walipotembelea hifadhi ya taifa
Ndugu zetu wakiwa ndani ya gari linalokokotwa na farasi ikiwa sehemu ya maonyesho ya kihistoria ya mji wa karne ya 19 wa Amerika ya Kaskazini
Watumishi wa wakati wote waliofika kwenye kusanyiko hilo wakitembea uwanjani baada ya programu kwisha Jumapili jioni