Hamia kwenye habari

AGOSTI 20, 2020
MAREKANI

Radi na Upepo Mkali Wasababisha Uharibifu Mkubwa Magharibi mwa Marekani

Radi na Upepo Mkali Wasababisha Uharibifu Mkubwa Magharibi mwa Marekani

Eneo

Magharibi mwa Marekani

Janga

  • Agosti 10, 2020, radi kubwa na pepo kali zilivuma kwa kasi kutoka sehemu moja hadi nyingine ya nchi. Dhoruba ya aina hiyo huitwa derecho.

  • Upepo huo uliharibu mali na mazao na kusababisha umeme ukatike katika maeneo makubwa

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri 2 walipata majeraha madogo

  • Wahubiri 18 walilazimika kuhama makao yao

Uharibifu wa mali

  • Nyumba 216 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 5 zilipata uharibifu mkubwa

  • Majumba ya Ufalme 24 yaliharibiwa kidogo

Jitihada za kutoa msaada

  • Halmashauri za Kutoa Msaada katika eneo hilo zinashirikiana na waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa ili kuwaandalia ndugu na dada mahitaji yao

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza ndugu na dada zetu katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na dhoruba hiyo, nasi tunaendelea kutazamia wakati ambapo hakuna mtu atakayekuwa na hofu ya kupoteza nyumba yake kutokana na majanga ya asili.—Isaya 65:21.