Hamia kwenye habari

Magari yaliyo kwenye njia iliyofurika maji mbele ya nyumba ya Mashahidi katika eneo la Harlingen, Texas

JULAI 10, 2019
MAREKANI

Upepo Mkali na Mafuriko Yapiga Kusini mwa Texas

Upepo Mkali na Mafuriko Yapiga Kusini mwa Texas

Juni 24, 2019, kulikuwa na upepo mkali na mvua kubwa kusini mwa Texas. Vyombo vya habari vilitangaza kwamba mamia ya nyumba yalijaa maji na zaidi ya watu 100 walihamishwa.

Ingawa hakuna wahubiri waliojeruhiwa na dhorubu hiyo, wahubiri 47 kati yao wamehamishwa. Kwa kuongezea, dhoruba hiyo iliharibu nyumba 65 za ndugu na dada zetu, na jengo moja la makazi lililopakana na Jumba la Ufalme.

Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo wanafanya ziara za uchungaji kwa wale walioathiriwa na dhoruba hiyo. Na halmashauri ya kutoa msaada inasimamia mipango ya makao, kugawa chakula, maji, na mavazi. Mpango wa kusafisha na kurekebisha nyumba za akina ndugu na jengo lililopakana na Jumba la Ufalme inaendelea.

Tutaendelea kuwatia moyo ndugu na dada zetu walio kusini mwa Texas, wanapoendelea kumtumaini Yehova na kushughulika na matokeo ya dhoruba hiyo.—Isaya 26:3, 4.