Hamia kwenye habari

Eneo la McKinney, Texas, baada ya kupigwa na vimbunga

MACHI 1, 2021
MAREKANI

Vimbunga Vyapiga Kusini mwa Marekani na Kusababisha Watu 7,500 Wakose Makazi kwa Muda

Vimbunga Vyapiga Kusini mwa Marekani na Kusababisha Watu 7,500 Wakose Makazi kwa Muda

Eneo

Kusini mwa Marekani

Janga

  • Vimbunga vilipiga sehemu kubwa ya kusini mwa Marekani kuanzia Februari 13, 2021. Jimbo la Texas liliathiriwa zaidi. Barafu na baridi kali ilisababisha nyumba na biashara zikose umeme, na kuleta uharibifu mkubwa wa mabomba yaliyoganda kwa sababu ya barafu

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri 11 walihitaji kutibiwa hospitalini

  • Wahubiri 94 walijeruhiwa kidogo

  • Wahubiri 7,650 walilazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa mali

  • Majumba 14 ya Ufalme na Jumba 1 la Kusanyiko liliharibiwa kidogo

  • Majumba 5 ya Ufalme yaliharibiwa vibaya

  • Nyumba 3,224 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 113 ziliharibiwa kwa kadiri kubwa

  • Nyumba 12 ziliharibiwa kabisa

Jitihada za kutoa msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanafanya kazi pamoja na Halmashauri ya Kutoa Msaada ya eneo hilo inayoshughulikia ugonjwa wa COVID-19 ili kutoa msaada kama vile, kugawa maji safi ya kunywa na kurekebisha nyumba na Majumba ya Ufalme. Ndugu hao waliwatafutia pia makazi ya muda wale ambao walilazimika kuhama makazi yao. Jitihada zote za kutoa msaada zinazingatia miongozo ya kujilinda dhidi ya COVID-19

Tunathamini kwamba Yehova anatoa faraja kwa wale wanaoathiriwa na majanga hayo ya asili.—2 Wakorintho 1:3.