Hamia kwenye habari

DESEMBA 14, 2021
MAREKANI

Vimbunga Vyasababisha Uharibifu Mkubwa Katika Maeneo ya Kusini na Sehemu za Kati za Marekani

Vimbunga Vyasababisha Uharibifu Mkubwa Katika Maeneo ya Kusini na Sehemu za Kati za Marekani

Kuanzia Desemba 10, 2021, vimbunga kadhaa vilipita kusini na katikati ya Marekani. Vilisababisha uharibifu mkubwa katika eneo lenye urefu wa kilometa 402. Watu kadhaa walikufa, wengine wengi wakapoteza makao yao, na majengo mengi yaliharibiwa. Jimbo la Kentucky ndilo lililoathiriwa zaidi.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu aliyejeruhiwa au kuuawa

  • Wahubiri 31 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 10 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 3 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 9 ziliharibiwa kabisa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanazifariji familia zilizoathiriwa

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinatolewa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya COVID-19

Tuna uhakika Yehova anawahurumia sana ndugu na dada ambao wanateseka kutokana na misiba hiyo ya asili.​—Isaya 63:9.