Hamia kwenye habari

NOVEMBA 1, 2017
MAREKANI

Mashahidi wa Yehova Wauza Majengo ya Kihistoria, The Towers

Mashahidi wa Yehova Wauza Majengo ya Kihistoria, The Towers

NEW YORK—Oktoba 31, Mashahidi wa Yehova waliuza jengo lao lenye orofa 16 katika Mtaa wa 21 wa Clark katika Wilaya ya Kihistoria ya Brooklyn. Kwa zaidi ya miaka 40, Mashahidi walitumia na kudumisha jengo hilo lililokuwa hoteli.

Jengo walilonunua liliitwa Leverich Towers Hotel na lilifunguliwa mwaka wa 1928. Muda mfupi baadaye, liliitwa Towers Hotel, na kwenye matangazo ya kibiashara lilitajwa kuwa “Hoteli ya Kifahari Zaidi Brooklyn,” na ilitembelewa na watu mashuhuri sana. Hata hivyo, kufikia miaka ya 1970 lilikuwa limechakaa kwa kiasi fulani.

Mashahidi walinunua jengo hilo mwaka wa 1975, ingawa walikuwa wamekodi orofa kadhaa kwa ajili ya familia ya makao makuu iliyoongezeka. Jengo hilo lilirekebishwa mara mbili wakati linamilikiwa na Mashahidi: kwanza mwaka wa 1978, na tena mwaka wa 1998.

David A. Semonian, msemaji wa Mashahidi wa Yehova, anasema hivi: “Sisi tulioishi Brooklyn Heights, tunakumbuka majengo hayo si kama majengo ya kihistoria bali kama makao maridadi na yenye kustarehesha. Kwa kuuza jengo hilo ni kama tumefunga sehemu fulani ya historia ya Brooklyn.”

Katika 2016, makao makuu ya Mashahidi wa Yehova yalihamishiwa Warwick, New York.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000