OKTOBA 17, 2018
MAREKANI
Kimbunga Michael, Mojawapo ya Dhoruba Kali Zaidi Katika Historia ya Marekani, Yasababisha Uharibifu Mkubwa
Oktoba 10, 2018, Kimbunga Michael kilitokea katika jimbo la Florida na kutokeza uharibifu mkubwa katika eneo la kusini-mashariki mwa Marekani. Kimbunga hicho kinaonekana kuwa mojawapo ya dhoruba kali zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani na kimesababisha uharibifu mkubwa sana wa mali. Kimbunga hicho pia kimesababisha vifo vya angalau watu 18.
Kimbunga hicho kiliwaathiri ndugu na dada katika makutaniko 94 na mizunguko 13. Hakuna yeyote kati ya ndugu zetu aliyekufa kutokana na dhoruba hiyo, lakini watatu walijeruhiwa. Dhoruba hiyo iliharibu nyumba 528 za akina ndugu na Majumba 34 ya Ufalme. Umeme katika jumla ya Majumba 39 ya Ufalme ulikatwa.
Ofisi ya tawi ya Marekani inaratibu kazi ya kutoa msaada, ikisaidiwa na Halmashauri ya Kutoa Msaada Wakati wa Misiba na zaidi ya waangalizi 40 wa mzunguko. Kazi hiyo inatia ndani kuwasambazia akina ndugu chakula, msaada wa kitiba, kuwaandalia makao, na maji, kutia ndani kuimarisha nyumba za akina ndugu kwa kufunika paa kwa turubai na kuondoa uharibifu mkubwa uliotokezwa na miti iliyoanguka. Pia mipango imefanywa ili kuwaimarisha kiroho na kuwafanyia akina ndugu na dada ziara za uchungaji.
Ingawa waabudu wenzetu wanaathiriwa na hali nguvu za mfumo huu, kutia ndani misiba ya asili, wanamtegemea Mungu wetu ili awape utegemezo wa kuendelea.—Zaburi 142:5.