Hamia kwenye habari

NOVEMBA 8, 2017
MAREKANI

Mashahidi Wauza Eneo la 74 Adams, Mojawapo ya Maeneo Yaliyosalia Yanayoweza Kuendelezwa Katika Dumbo, Brooklyn

Mashahidi Wauza Eneo la 74 Adams, Mojawapo ya Maeneo Yaliyosalia Yanayoweza Kuendelezwa Katika Dumbo, Brooklyn

Jumanne, Novemba 7, Mashahidi wa Yehova waliuza eneo la 74 Adams Street, lililo kwenye eneo la kihistoria la Dumbo lililoko Brooklyn, New York. Ni mojawapo ya maeneo ya mwisho katika eneo la Dumbo.

Mashahidi walinunua eneo hilo mwaka wa 1975 na wakajenga gereji mwaka wa 1976 ili kudumisha magari yao. Walipanua jengo hilo katika mwaka wa 1990 na hivyo likawa na ukubwa unaokaribia mara mbili ya jinsi lilivyokuwa awali. Eneo hilo lina mita 2,236 za mraba na lina nafasi yenye ukubwa wa mita 13,462 za mraba ambazo zinaweza kutumiwa katika upanuzi mwingine. Eneo hilo litatumiwa kwa njia kadhaa kama vile kufanywa kuwa eneo la kuegesha magari, eneo la makazi, na biashara.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000