Hamia kwenye habari

MACHI 2, 2018
MAREKANI

Mafuriko Yaathiri Eneo la Kati la Marekani

Mafuriko Yaathiri Eneo la Kati la Marekani

Katika mwezi wa Februari 2018, mvua kubwa pamoja na theluji iliyoyeyuka ilisababisha mafuriko eneo la kati la Marekani. Ndugu na dada zetu katika maeneo fulani ya Illinois, Indiana, Kentucky, Michigan, Ohio, na Tennessee walikuwa kati ya walioathiriwa na mafuriko hayo.

Ofisi ya Marekani inaripoti kwamba wahubiri 20 katika mizunguko minane wamelazimika kuhama nyumba zao. Inasikitisha kwamba dada mmoja katika eneo la Indiana alikufa wakati wa mvua kubwa zilizonyesha kabla ya mafuriko. Nyumba 57 zimeharibiwa.

Waangalizi wa mzunguko katika maeneo hayo wanawafariji wahubiri wote walioathiriwa na mafuriko hayo. Tunaendelea kuwakumbuka katika sala ndugu na dada zetu walioathiriwa, tukijua kwamba Yehova atashughulikia mahangaiko yao yote.—1 Petro 5:7.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000