Hamia kwenye habari

FEBRUARI 27, 2015
MAREKANI

Mashahidi Watunukiwa kwa Ujenzi Usioharibu Mazingira

Mashahidi Watunukiwa kwa Ujenzi Usioharibu Mazingira

NEW YORK—Mashahidi wa Yehova, wanaojulikana sana kwa sababu ya kazi ya ulimwenguni pote ya elimu ya Biblia, wanapongezwa kwa kujenga majengo mazuri yasiyoharibu mazingira.

Shirika la Majengo Yasiyoharibu Mazingira (GBI) lilitoa vyeti kwa majengo mawili mapya ya Mashahidi yaliyopo Wallkill, New York kwenye ofisi ya tawi ya, Marekani: Jengo la Makazi F kwenye Mashamba ya Watchtower, lililokamilika mwishoni mwa mwaka 2012, na Jengo la Ofisi la Watchtower Wallkill, lililokamilika mwaka wa 2014. Majengo hayo mawili yalipokea tuzo ya juu zaidi ya Four Green Globes.

Majengo ya Ofisi ya Watchtower Wallkill

Shaina Sullivan, Mkurugenzi wa Masokowa shirika la GBI, alisema hivi: “Ulimwenguni pote, kati ya majengo yote yaliyokaguliwa ni chini ya asilimia 4 tu ya majengo kwenye programu hiyo ndiyo yaliyotunukiwa cheti hicho cha Four Green Globes.” Bi. Sullivan aliongezea kwamba Jengo la Ofisi la Watchtower Wallkill “ndio mradi wa kwanza usio wa makazi katika jimbo la New York kupata cheti hicho.” Jenna Middaugh, Mkurugenzi wa Miradi wa GBI, alisema hivi: “Kati ya majengo 23 [nchini Marekani] ambayo yamepewa cheti cha Four Green Globes tangu mwaka wa 2006, Jengo la Ofisi ya Watchtower Wallkill ndilo lililopata alama ya juu zaidi ya asilimia 94.”

Jengo la Makazi F kwenye Mashamba ya Watchtower

GBI husimamia shirika la Green Globes kama shirika la kukadiria na kutoa vyeti ambavyo vinatumia maoni ya kikundi cha tatu katika eneo la ujenzi kukagua ubora wa majengo. Ili kupata vibali vya Green Globes majengo yanahitaji kuwa yasiyoharibu mazingira kwa njia ya kutunza maji, kupunguza matumizi ya nishati na gesi zinazoongeza joto duniani, kupunguza matumizi ya mali asili kwa kutumia vifaa vinavyofaa, na kutengeneza mazingira mazuri ndani ya jengo.

Mabamba ya kutokeza umeme kwa kutumia nguvu za jua hutokeza angalau asilimia 10 ya umeme unaotumika katika Jengo la Ofisi la Watchtower Wallkill, ni moja ya mambo yaliyofanya wakapata tuzo.

David Bean, mratibu wa miundo ya udumishaji wa majengo ya Mashahidi nchini Marekani, anasema hivi: “Kupata tuzo hizo kunathibitisha jinsi miundo na majengo ya miradi yetu yote ilivyo ya kiwango cha juu. Tungependa pia kupata vyeti vya Green Globes katika miundo na ujenzi ya makao yetu makuu mapya ya Warwick, New York.”

Kuweka paa linalotunza mazingira, ambalo ni moja ya miundo ya udumishaji katika majengo ya makao makuu mapya ya Mashahidi katika Warwick, New York.

Zeny St. Jean, anayeratibu miradi ya ujenzi ya Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote, alisema hivi kutoka makao makuu ya ulimwenguni pote: “Ingawa lengo letu kuu ni elimu ya Biblia, tunathamini tuzo hizo kwa sababu zinaonyesha kwamba tunajenga majengo yasiyoharibu mazingira, jambo ambalo tunajaribu kufanya katika majengo yetu yote ulimwenguni pote.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000