Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Marekani
JUNI 17, 2002—Mahakama Kuu ya Marekani yaunga mkono uamuzi uliofanywa na mahakama hiyo katika miaka ya 1940 iliyowapa Mashahidi wa Yehova haki ya kisheria ya kuhubiri hadharani (Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc. v. Village of Stratton)
AGOSTI 1998—Idadi ya Mashahidi wa Yehova yazidi milioni moja
APRILI 15, 1992—Katika kesi ya Pater v. Pater, Mahakama Kuu ya Ohio yaunga mkono uamuzi wa mahakama ya juu na kutangaza kwamba mahakama ya chini ilitoa uamuzi ulio kinyume na sheria wa kumnyang’anya mzazi watoto wake kwa msingi wa dini yake
OKTOBA 30, 1985—Mahakama Kuu ya Mississippi yaamua kwamba uamuzi wa kutiwa damu mishipani ni wa mtu binafsi kwa sababu ana haki ya faragha na ya dini (In re Brown)
AGOSTI 31, 1972—Mahakama ya Rufaa ya Wilaya ya Columbia yaamua kwamba jimbo linapaswa kuheshimu haki za watu wazima ambao ni timamu wanapokataa kutiwa damu mishipani (In re Osborne)
NOVEMBA 30, 1953—Mahakama Kuu ya Marekani yaamua kwamba licha ya kufanya kazi ya kimwili, Shahidi wa Yehova anayetumika akiwa mtumishi wa wakati wote ana haki ya kutojiunga na jeshi (Dickinson v. United States)
1944—Kuteswa kwa Mashahidi wa Yehova kunapungua
JUNI 14, 1943—Mahakama Kuu ya Marekani yabadili uamuzi uliotolewa awali katika kesi ya Gobitis na kutangaza kwamba ni kinyume na sheria kumlazimisha mwanafunzi ambaye ni Shahidi kusema kiapo cha uaminifu na kusalimu bendera (West Virginia State Board of Education v. Barnette)
MEI 3, 1943—Mahakama Kuu ya Marekani yafuta sheria iliyotaka Mashahidi wa Yehova walipie kibali cha kutoa machapisho ya kidini (Murdock v. Pennsylvania)
JUNI 3, 1940—Mahakama Kuu ya Marekani yaunga mkono agizo kwamba wanafunzi wanapaswa kusalimu bendera (Minersville School District v. Gobitis); Mashahidi waanza kuteswa baada ya hapo
MEI 20, 1940—Kwa mara ya kwanza Mahakama Kuu ya Marekani yaamua kwamba majimbo na wenye mamlaka wanapaswa kuheshimu Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani kuhusiana na suala la uhuru wa kidini. Kwa kuongezea, Mahakama yaamua kwamba huduma ya Mashahidi wa Yehova haichochea vurugu (Cantwell v. Connecticut)
MACHI 28, 1938—Mahakama Kuu ya Marekani yafuta sheria iliyotaka Mashahidi waombe kibali kabla ya kugawa machapisho (Lovell v. City of Griffin)
JULAI 26, 1931—Wanafunzi wa Biblia wabadilisha jina kuwa Mashahidi wa Yehova
MEI 14, 1919—Mashtaka ya washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania yabadilishwa; baadaye mashtaka hayo yaliondolewa
JUNI 20, 1918—Washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania wakamatwa na kufungwa gerezani kwa madai ya kwamba walichapisha habari ambazo zinapinga jitihada za vita
MACHI 4, 1909—Shirika la kisheria lililoitwa Peoples Pulpit Association linaanzishwa kisha baadaye linabadilishwa jina na kuitwa Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.
JANUARI 31, 1909—Wanafunzi wa Biblia wanahamishia makao makuu Brooklyn, New York
DESEMBA 15, 1884—Shirika la kisheria laanzishwa na baadaye likaitwa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
Miaka ya 1880—Wanafunzi wa Biblia wafungua ofisi ya makao makuu huko Allegheny, Pennsylvania
JULAI 1879—Toleo la kwanza ya gazeti ambalo sasa linafahamika kwa jina Mnara wa Mlinzi linatolewa
1870—Charles Taze Russell na wenzake waanzisha kikundi cha kujifunza Biblia huko Allegheny, Pennsylvania, na baadaye kikundi hicho kinajulikana kwa jina Wanafunzi wa Biblia