Hamia kwenye habari

OKTOBA 13, 2017
MAREKANI

RIPOTI YA KWANZA | Moto wa Msituni wa California

RIPOTI YA KWANZA | Moto wa Msituni wa California

Halmashauri ya Tawi ya Marekani imetoa habari zifuatazo kuhusu ndugu zetu walioathiriwa na moto Kaskazini mwa California, na wale walioathiriwa na moto uliosambaa haraka Kusini mwa California.

California Kaskazini: Ofisi ya tawi ya Marekani imewasiliana na waangalizi wa mzunguko katika majimbo ya Mendocino, Napa, Sonoma, pamoja na maeneo jirani, na waliripoti kwamba ndugu wote wako salama, ingawa mhubiri mmoja alijeruhiwa. Ndugu zetu 700 hivi wamelazimika kuhama, na wengine 2,000 hivi wako tayari kuhama ikiwa kutakuwa na uhitaji. Ndugu zetu wote waliokimbia maeneo hayo wamepata makao kwa akina ndugu wanaoishi maeneo salama zaidi. Kufikia sasa, tumethibitisha kwamba Jumba moja la Ufalme na nyumba tatu za akina ndugu zimeharibiwa. Isitoshe, nyumba 22 zimeathiriwa sana na nyingine 32 zimeathiriwa kidogo. Waangalizi wa mzunguko wanaongoza mambo ili kuwatia moyo na kuwategemeza akina ndugu.

California Kusini: Katika eneo la Anaheim, familia 25 za Mashahidi zimelazimika kuhama, hakuna ndugu aliyejeruhiwa. Familia hizo zote zinaishi katika nyumba za Mashahidi wenzao. Hakuna nyumba au Majumba ya Ufalme yaliyoripotiwa kwamba yameharibiwa.

Tuna uhakika kwamba Yehova atakuwa “kimbilio salama” kwa wote walioathiriwa katika kipindi hiki kigumu.—Zaburi 9:9, 10.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000