Hamia kwenye habari

AGOSTI 17, 2020
MEXICO

Kimbunga Hanna Chasababisha Uharibifu Nchini Mexico

Kimbunga Hanna Chasababisha Uharibifu Nchini Mexico

Mahali

Majimbo ya Tamaulipas na Nuevo León nchini Mexico

Janga

  • Julai 26, 2020, Kimbunga Hanna, kilileta dhoruba iliyopiga maeneo ya kaskazini-mashariki mwa Mexico na kusababisha mafuriko makubwa

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Katika jimbo la Nuevo León, familia 14 zilihamishwa kabla ya dhoruba hiyo kuanza

  • Katika jiji la Reynosa, kwenye jimbo la Tamaulipas, wahubiri 100 walilazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa Mali

  • Nyumba 21 zimeharibiwa katika jimbo la Nuevo León

  • Nyumba 117 zimeharibiwa katika jimbo la Tamaulipas

Jitihada za kutoa msaada

  • Ofisi ya tawi ya Amerika ya Kati imeunda Halmashauri ya Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko katika maeneo yaliyoathiriwa wanashirikiana na wazee katika kuratibu zoezi la kusafisha na kuua vijidudu vya magonjwa katika nyumba zilizoathiriwa na mafuriko

  • Katika jimbo la Nuevo León, ndugu na dada wengi waliohama sasa wameweza kurudi nyumbani

  • Katika jimbo la Tamaulipas, makutaniko yanawapa chakula na nguo walioathiriwa na kimbunga hicho

Tunamshukuru Yehova kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa katika janga hilo. Kazi ya kutoa msaada iliyofanywa inaonyesha kwamba Baba yetu aliye mbinguni na watu wake ni “msaada unaopatikana kwa urahisi nyakati za taabu.”—Zaburi 46:1.