Hamia kwenye habari

NOVEMBA 2, 2023
MEXICO

Kimbunga Otis Kimesababisha Uharibifu Mkubwa Katika Pwani ya Kusini-magharibi mwa Mexico

Kimbunga Otis Kimesababisha Uharibifu Mkubwa Katika Pwani ya Kusini-magharibi mwa Mexico

Oktoba 25, 2023, Kimbunga Otis kilisababisha uharibifu mkubwa katika pwani ya kusini-magharibi mwa Mexico karibu na jiji la kitalii la Acapulco, nchini Mexico. Kimbunga hicho kiliongezeka ukubwa kwa kasi zaidi kuliko kimbunga kingine chochote ambacho kimewahi kutokea katika eneo hilo la Bahari ya Pasifiki. Hilo lilitokeza upepo mkali uliovuma kwa kilomita 265 kwa saa, mvua kubwa, na mafuriko makubwa. Ripoti zinaonyesha kwamba kuna uharibifu mkubwa wa barabara, majengo, na miundo mbinu. Maelfu ya watu wameachwa bila umeme. Watu 45 hivi wamekufa.

Zifuatazo ni ripoti za awali ambazo tumepata kutoka kwa akina ndugu wa eneo hilo.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada ambaye amekufa au kujeruhiwa

  • Zaidi ya ndugu na dada 10,000 wanaishi katika eneo lililoathiriwa

  • Jumba 1 la Ufalme limepata uharibifu mkubwa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wanaandaa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa wale walio katika eneo lililoathiriwa

  • Wawakilishi 4 kutoka ofisi ya tawi ya Amerika ya Kati walitembelea eneo lililoathiriwa ili kuwatia moyo na kuwategemeza ndugu na dada zetu

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada imewekwa rasmi ili kusimamia jitihada za kutoa msaada

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwapa amani na faraja ndugu na dada zetu wapendwa ambao wameathiriwa na Kimbunga Otis.​—Wafilipi 4:6, 7.