NOVEMBA 3, 2021
MEXICO
Kimbunga Pamela Chasababisha Mafuriko Katika Pwani ya Pasifiki ya Mexico
Oktoba 13, 2021, Kimbunga Pamela kilipiga eneo la pwani ya Mexico. Kimbunga hicho kilitokeza upepo mkali, mvua kubwa, na mafuriko hasa katika maeneo ya Durango, Nayarit, na Sinaloa.
Athari kwa Ndugu na Dada Zetu
Hakuna yeyote kati ya ndugu zetu aliyejeruhiwa
Wahubiri 112 walilazimika kuhama nyumba zao
Nyumba 75 zilipata uharibifu mdogo
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Ndugu zetu wanasema kwamba walikuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kimbunga hicho kwa sababu ya vikumbusho vinavyotolewa na tengenezo letu kuhusiana na misiba ya asili
Waliolazimika kuhama nyumba zao wamepata mahali pa kulala katika nyumba za watu wa ukoo au Mashahidi wenzao
Wahubiri 20 walipewa msaada wa chakula
Wazee wa eneo hilo wanawafanyia ziara za uchungaji wale walioathiriwa
Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya usalama ya COVID-19
Upendo wa Yehova kuwaelekea ndugu zetu unaonekana wazi kutokana na jitihada za kutoa msaada zilizotolewa upesi sana. Kwa kweli Mungu wetu ni ‘kimbilio salama.’—Zaburi 59:16.