SEPTEMBA 12, 2017
MEXICO
Dhoruba Lidia Yapiga Mexico
Dhoruba Lidia ilipiga Rasi ya Mexico ya Baja California siku ya Ijumaa, Septemba 1. Ingawa ilipungua nguvu kufikia Jumamosi, dhoruba hiyo ilisababisha mvua kubwa inyeshe ambayo ilifikia kiwango cha sentimita 69 za ujazo, kiwango kikubwa zaidi kuwahi kuripotiwa tangu mwaka wa 1933. Watu watano hivi wamekufa kutokana na dhoruba hiyo.
Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Mexico City, inaripoti kwamba dada mmoja alikufa baada ya kusombwa na maji alipokuwa akitembea kuelekea nyumbani. Wengine watatu waliokolewa baada ya kukutwa wakiwa wamezingirwa na maji . Isitoshe, nyumba nane ziliharibiwa na dhoruba hiyo. Waathiriwa wote wanatunza na watu wa familia au Mashahidi wenzao.
Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia kazi ya kutoa msaada kutoka makao makuu ya ulimwenguni pote, wakitumia michango iliyotolewa katika kazi ya ulimwenguni pote ya kuhubiri.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000
Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52-555-133-3048