Hamia kwenye habari

OKTOBA 29, 2014
MEXICO

Mashahidi wa Yehova Nchini Mexico Wawasaidia Walioathiriwa na Kimbunga Odile

Mashahidi wa Yehova Nchini Mexico Wawasaidia Walioathiriwa na Kimbunga Odile

Baada ya Kimbunga Odile kuipiga pwani ya Baja California Sur Jumatatu, Septemba 15, 2014, Mashahidi wa Yehova katika eneo la karibu waliwapelekea washiriki wao walioathiriwa chakula, maji, na dawa. Tangu mwaka wa 1967, hakujawahi kuwa na dhoruba kali zaidi ya hiyo lakini hakuna Shahidi aliyekufa au kujeruhiwa. Hata hivyo, dhoruba hiyo ilibomoa kabisa nyumba 82 za Mashahidi na kuharibu nyingine 85, na familia 125 zililazimika kuhama. Walipata makao katika nyumba za Mashahidi wenzao. Siku nne kabla ya kimbunga hicho, halmashauri za kutoa msaada za Mashahidi zilituma barua kwenye makutaniko katika eneo hilo zilizoonyesha mambo ya kufanya ili kujitayarisha kwa ajili ya kimbunga hicho. Wazee katika makutaniko hayo walipanga kuwahamisha Mashahidi wengine walioishi katika nyumba zinazoweza kuporomoka kwa urahisi wakaishi na wenzao. Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Mexico ilituma zaidi ya tani 20 za msaada katika eneo hilo lililokumbwa na msiba.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52 555 133 3048