Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 8, 2017
MEXICO

Tetemeko la Nchi Lapiga Mexico

Tetemeko la Nchi Lapiga Mexico

Siku ya Alhamisi, Septemba 7, tetemeko la nchi la kiwango cha 8.2 lilipiga pwani ya kusini ya Pasifiki ya Mexico. Tetemeko hilo ndilo kubwa zaidi kuwahi kupiga Mexico kwa kipindi cha karne moja na liliua watu 45 hivi. Kwa kusikitisha tumepata ripoti kwamba ndugu mmoja na dada wawili walikufa.

Pia, ripoti zinaonyesha kwamba nyumba nyingi za akina ndugu na Majumba ya Ufalme kadhaa yameharibiwa. Majumba mawili ya kusanyiko katika Jimbo la Chiapas yaliharibiwa pia. Uchunguzi unaendelea kuhakikisha kiwango cha uharibifu.

Tunaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu, tukiwa na uhakika kwamba Yehova atawafariji na kuwaimarisha.—2 Wathesalonike 2:16, 17.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52-555-133-3048