Hamia kwenye habari

Kimbunga Chalane chapiga pwani ya Msumbiji

JANUARI 13, 2021
MSUMBIJI

Kimbunga Chalane Chapiga Msumbiji

Kimbunga Chalane Chapiga Msumbiji

Eneo

Majimbo ya Sofala na Manica yaliyo katika eneo la kati la Msumbiji, kutia ndani maeneo ambayo tayari yaliharibiwa na Kimbunga Idai kilichotokea Machi 2019

Janga

  • Kimbunga Chalane kilipiga pwani ya Msumbiji Desemba 30, 2020. Mafuriko na maporomoko ya ardhi yalisababisha uharibifu mkubwa katika maeneo mengi

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri watatu walijeruhiwa kidogo

Uharibifu wa mali

  • Nyumba 34 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 12 ziliharibiwa kwa kadiri kubwa

  • Nyumba 16 ziliharibiwa kabisa

  • Majumba 7 ya Ufalme yaliharibiwa kidogo

  • Majumba 4 ya Ufalme yaliharibiwa kwa kadiri kubwa

  • Jumba 1 la Ufalme liliharibiwa kabisa

Jitihada za kutoa msaada

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada iliwekwa rasmi ili kuratibu jitihada za kutoa msaada zilizotia ndani kuwatafutia makazi ya muda wahubiri ambao makazi yao yaliharibiwa. Jitihada zote za kutoa misaada huratibiwa kwa kuzingatia miongozo ya kujilinda na COVID-19

Tunasali kwamba Yehova ataendelea kuwasaidia ndugu na dada zetu walioathiriwa na kimbunga hicho.—Zaburi 121:2.